BASHUNGWA AKERWA NA KASI NDOGO UJENZI WA MSALATO AIRPORT
Wizara ya Ujenzi Wizara ya Ujenzi
5.41K subscribers
2,393 views
16

 Published On Sep 29, 2023

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, ameagiza kampuni ya Beijing Construction Engineering Group kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa jengo la abiria na jengo la kuogozea ndege katika Kiwanja cha Kimataifa cha Msalato, Dodoma ifikapo Desemba, 2024 kulingana na maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Bashungwa amesema hayo leo Septemba 28, 2023 jijini Dodoma wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho na kutokuridhishwa na kasi ya maendeleo yake kutokana na kusuasua kwa mkandarasi huyo. "Mkandarasi usivimbe kichwa kana kwamba umepata kazi nyingi, usipozingatia maelekezo ambayo nimekupatia, kulingana na vipengele vilivyopo kwenye mkataba, tunaweza kukusimamisha kazi kwa mujibu wa sheria " amesema Bashungwa.

Amemtahadharisha Mkandarasi huyo iwapo atazembea kukamilisha kazi hiyo kwa wakati itampelekea kutopata kazi nyingine katika Sekta ya Ujenzi ndani ya nchi.

#viral #news #ujenzi

show more

Share/Embed