Seneta Mutula afanyiwa upasuaji mdogo baada ya kusakamwa na chakula
NTV Kenya NTV Kenya
2.5M subscribers
15,119 views
37

 Published On Sep 26, 2018

Seneta wa Makueni, Mutula Kilonzo Junior kusalia hospitalini ili kupokea matibabu zaidi baada ya kusakamwa na chakula katika mkahawa mmoja huko Nandi. Mutula Jr amelazwa katika hospitali ya mafunzo na rufaa ya Moi mjini Eldoret.
Seneta Kilonzo ambaye yuko ziarani kaunti ya Nandi kwa hisani ya seneta wa Nandi Samson Cherargei walikuwa wameandamana katika bunge la Nandi ambapo Cherargei alikuwa akuhutubia bunge hilo kuhusu maswala ya kaunti hiyo. Inasemekana baada ya mkutano huo Mutula Jr alikwenda kutafuta chamcha katika mkahawa mmoja eneo hilo, alipopaliwa na chakula. Kwa mujibu wa afisa mkuu mtendaji katika hospitali ya mafunzo na rufaa ya Moi daktari Wilson Aruasa, amedhibitisha tukio hilo na kusema Mutula Jr yuko katika hali nzuri na ataruhusiwa kwenda nyumbani baada ya matibabu. Haya yakijiri kikao cha maseneta kinaendelea katika kaunti ya Uasin Gishu.

show more

Share/Embed