Ambwene Mwasongwe - Nifundishe Kuomba (Official Music Video)
Ambwene Mwasongwe Ambwene Mwasongwe
181K subscribers
242,150 views
3.3K

 Published On Premiered Apr 4, 2023

Ambwene Mwasongwe Presents the Music Video for "Nifundushe Kuomba"

Maelezo ya wimbo wa Nifundishe Kuomba:

Nifundishe kuomba ni neno lenye uhitaji wa mtu aliyeguswa na Roho Mtakatifu na akagundua kuna namna mambo hayaendi sawa kwa sababu mbalimbali.

Unaweza kuwa unaomba lakini swali ni unaombaje? na ukigundua unaomba vibaya lazima urudi na umuombe akufundishe kuomba ili uombe sawasawa na mapenzi yake.

Upande wangu niliomba nifundishwe kuomba nikiwa na mahusiano ya ndani sana na ya karibu ili kuomba kwangu kusizuiliwe.

Ni wimbo wa baraka ambao natamani unaposikia upate neema ya kufundishwa kuomba pia.

Watch All Music Videos by Ambwene Mwasongwe:    • Ambwene Mwasongwe All Music Videos  

Follow Ambwene Mwasongwe
Instagram:   / ambwenemwasongwe_  

Subscribe to Ambwene Mwasongwe:    / @ambweneobadiamwasongwe  

Digital Branding & Marketing By:
Black Ozen Entertainment Limited:   / blackozenentertainmentlimited  

Ambwene Mwasongwe - Nifundishe Kuomba (Lyrics)

Jina lako messiah
Hili ni ombi langu,
Nifundishe kuomba
Nifundishe kunena,
Nifundishe kiasi
Nifundishe imani ya
Matendo, nipe moyo wa toba

Nautaka uwepo unakoishi
, Ambako wewe ni kichwa
Cha kanisa.
Nazitaka nguvu
Ulizonazo wewe,
Ninataka upako
Maneno yangu, matendo
Yangu, tabia yangu,
Zifanane na hisia zako.

Nikitembea nitembee
Na wewe Yesu,
Ninataka kushinda aaaiii
Nami nakusalute
Eeeh master
Ninakuimbia wimbo,
Ninapaza sauti
Nami na kusifu,
Kuhani wa ubora.

Mmiliki halali kwa
Agano la neem.
Jina lako ni messiah
Hili ni ombi langu,
Nifundishe kuomba
Nifundishe kunena,
Nifundishe kiasi
Nifundishe imani ya
Matendo, nipe
Moyo wa toba
Ndani ya moyo
Wangu, ninataka
Uishi wewe bwana

Wa wema
Uewezae kuuzuia
Ulimi wangu,
Usinene sawasawa
Na hasira zangu
Uewezae kuituliza
Akili yangu,
Isichanganyikiwe
Wakati wa raha
Uwezae kunituliza
Wakati wa shida na
Matatizo.

Wakati wengine
Wakimbiapo, ukanipe
Jibu la mbio zao.
Nguvu yako ikanizuie
Kwenda pale hakuna
Awezae niona,
Pale ambapo
Hayupo awezae
Sema acha, neno
Lako likanizuie kufanya.

Neema yako
Ikanifanye kupakua
Chakula tofautu
Na njaa yangu.
Kule nisikoweza
Kwenda mchana,
Nisaidie nisiende usiku.
Yale nisiyoweza
Sema hadharani,
Nisiseme gizani.
Nautaka uso wako
Kama wa chuma
Vinyamkela wasioweza
Kuustahimili.

Naitaka lugha ya
Kimbingu, isiyoneneka
Isiyonenwa na mtu.
Natamani mbingu
Za mbingu kwenye
Neema, kule Paulo
Alipoogelea nguvu zako.
Nikitembea, nitembee
Na wewe Yesu.
Ninataka kushinda aaaaiiii
Nitakanyaga mahali waoga hawapawezi.

Nitafanya ubabe
Kwenye ulimwengu
Wa roho
Nitapitisha mkong'oto
Kwenye mikwamo.
Nitaonyesha jeuri
Kwa shetani
Maana ufalme
Nauteka oooo
Unatekwa na wenye

Nguvu aiiiii
Nami nakusalute
Ninakuimbia wimbo,
Ninapaza sauti
Nami nakusifu,
Kuhani wa ubora
Mmiliki halali wa
Agano la neema
Jina lako ni Messiah
Hili ni ni ombi langu,
Nifundishe kuomba
Nifundishe kunena,
Nifundishe kiasi
Nifundishe imani
Ya matendo, nipe
Moyo wa toba.

#AmbweneMwasongwe #NifundisheKuomba

show more

Share/Embed