Neema Gospel Choir - Nikurejeshee Inspired by a True Story
Neema Gospel Choir Neema Gospel Choir
155K subscribers
41,228 views
834

 Published On Feb 10, 2024

Mnamo mwaka 2022, Familia ya Ev. Mchome, ilipitia kipindi kigumu sana baada ya kumpoteza mama yao mpendwa (Aliyeanguka ghafla na kufariki). Majonzi na simanzi kubwa ilitanda mioyoni mwao mithili ya wingu zito na giza totoro, hakuna maneno mazuri ambayo yangetosha kuwapa faraja familia hii.

Katikati ya giza hilo totoro, Ilipenyeza Nuru angavu mithili ya jua liangazavyo kutoka mashariki kwenda magharibi kabla ya machweo, Herman Mchome (Kiongozi wa Wimbo & Mwandishi wa wimbo huu) Akiwa nyumbani na kaka yake aitwaye Elisha Mchome aliyekuwa ameketi katika kiti na mwenye majonzi sana asijue ni nini kitafuata na nini atafanya. Wakati akipiga kinanda, akacheza ghani yenye hisia kubwa ndani yake ambayo ilizama mioyoni mwa wanafamilia hao na kuwapa faraja na tumaini jipya, Wakati huo Herman akiwa chumbani kwake, alihisi uzito ndani ya hisia zake, huzuni na majonzi vikiwa bado vimeiteka akili na moyo wake, ghafla! alisikia sauti ndani yake ikiongea naye Maneno haya. ”Nitarejesha vyote”

Ulikuwa ni mwanga wa ajabu uliopenyeza katikati ya giza nene na zito. Wimbo huu unazungumzia amani ya moyo ambayo haielezeki na furaha ile ambayo isingeweza kusababishwa na mwanadamu awaye yeyote yule pamoja na tumaini ambalo linatoka kwa Yesu pekee. Herman alipoanza kuimba wimbo huu aliumimina moyo wake kwa Yesu, Baba wa familia (Ev. Mchome) alisikia wimbo huo, ukaamsha hisia zake na kujiunga pamoja na wanaye hawa huku akiongeza maneno yake ya hekima kwenye wimbo.

Wimbo huu ulizaliwa katikati ya kina kirefu cha uchungu na majonzi mazito. Ulikuwa ufunuo wa ki-Mungu, ndipo ikawa sababu ya kurudisha furaha, amani ya moyo na maisha yenye tumaini kwa familia ya Ev. Mchome.

Herman ametuongoza katika wimbo huu, (Leader), Tumeimba kwa furaha yenye ushindi wa kishindo, tumaini na Imani isiyotikisika, Nuru inayong'aa katika giza nene.

Hakuna jambo linalomshinda MUNGU, hata kama kuna ugumu gani, yeye ana majibu.
“Amani yako iko kwa Yesu,
Furaha yako iko kwa Yesu,
Ushindi wako uko kwa Yesu,
Uzima wako uko kwa Yesu”

Anakurejeshea vyote vilivyoibiwa na yule mwovu.

show more

Share/Embed