Salama Na GODLIVER SE6 EP26 | LUVVIE PART 2 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460
YahStoneTown YahStoneTown
397K subscribers
61,425 views
757

 Published On Jul 19, 2022

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460

LUVVIE
Jina la episode litosheleze kumuelezea mgeni wetu wa wiki hii, hodari, mahiri, mcheshi na mwenye kujielewa ila kikubwa kuliko yote ni Mwanamke. Alipotoka na mipango yake ya maisha ilikua ni moja ya chachu zilizotufanya mimi na wenzangu tuone anastahili kukaa kitako kwenye kiti chetu kile kilichopauka. Na hakukua na mjadala juu ya yeye kuipata nafasi hii.

Godliver kwa sasa ndo nyota yetu ing’arayo kila kona ya bara na dunia kwa ujumla, kwa imani niliyonayo kwake naamini huu ni mwanzo tu wa mengi makubwa na mazuri na pengine ya kushangaza na kuiandikia historia Taifa letu yanakuja, kiu hiyo ya kupata hayo na zaidi unaiona kwenye macho yake na kujiamini alikonako. Ukibahatika na kuangalia kazi zake basi ndo utazidi kuamini na kumtakia kila lenye kheri.

Mitihani na kupanda na kushuka kwenye maisha yake naye alipitia kama kila mmoja wetu, jinsi alivyokua anayapangua na kutengeneza kinywaji kila mara alipokua anarushiwa malimao kumemfanya awe na kiu zaidi na kutaka kusonga mbele zaidi kwa kasi ya majaaliwa.
Alianza kama mas’hara tu na mengine ni historia tu kwa sasa. Mama wa mtoto mmoja ambaye ni kila kitu kwake, Godliver ananihadithia moja ya mikasa mingi ilowahi kumkuta maishani mwake, na pia amenikumbusha umuhimu wa kuchagua marafiki na watu ambao unawaweka karibu kwenye maisha yako.

Alishawahi kubadili dini na kuwa Muislamu, bahati nzuri alikua na wazazi ambao ni waelewa sana, hakuna aliyekua anamhukumu kwenye maamuzi yake, pengine walikua disappointed kwa kiasi fulani, zaidi Mzee wake lakini wala hakuonyesha kushutushwa au kutaka kumsema vibaya kwa maamuzi yake, badala yake waliheshimu na kumpa support tu kwenye maamuzi na maisha yake.
Maisha yamemumfundisha mengi tu, pengine kwa adhabu zaidi yamemfundisha kuwa marafiki ambao ndo aliwaona wanampenda sana waliishia kumhusisha na mambo ambayo si mazuri na ambayo yalimfanya ajaribu imani yake kwa kiasi kikubwa sana.

Humu anakumbuka jinsi alivyokua anahangaika kwa waganga na kujaribu kwa nguvu vitu ambayo vilikua hata havihitaji hiyo njia ambayo alikua anaaminishwa kama ndo zilikua sahihi.
Anakumbuka Imani yake ilivyo jaribiwa na utukufu wa Mungu alipokuja kumuongoza.
Hapo juu nilisema huyo ndo muigizaji BORA wa kike kwa sasa, pengine wengine wanaweza wakawa na mawazo tofauti kidogo na haikatazwi, ila kwenye vitabu vyangu? Kwa hesabu ya leo? Huyu ndo Mama yao.

Sasa aliwezaje kutoka huko? Alikutana vipi na Baba wa mtoto wake? Na filamu au kazi yake ya kwanza ilikua inatwaje? Na aliipataje hasa? Nani ndo anamuangalia sana maishani mwake? Ambaye angependa kuwa kama yeye? Wapi anajiona huko mbele kwenye kazi yake hii?
Natumai utajifunza mawili matatu kutoka kwa Dada Mkali na uta enjoy pia.

Love,
Salama.

Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs

Listen our Podcast on
Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa

Soundtrack Yeah by @MarcoChali    • Marco Chali Feat One The Incredible &...  

Follow:
Twitter:   / yahstonetown  
Instagram:   / yahstonetown  
Facebook:   / yahstonetown  

Channel Administered by Slide Digital
Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz

show more

Share/Embed